MY LIFESTYLE



Wote tunaelewa kuwa katika maisha, binadamu anamitindo mbalimbali ya kuishi, mitindo hii hutofautiana kati mtu na mtu, tukiweka kando hali zetu za kiuchumi, Lifestyle ni namna na jinsi mtu anavyo ishi, kwa lugha iliyonyepesi, jinsi mtu anavyo endesha maisha yake ya kila siku katika jamii inayo mzunguka.
Lifestyle pia yaweza kuwa ni tabia, mwonekano na mpangilio wa maisha yako kwa ujumla katika masuala mbalimbali ya kwako mwenyewe (within your own family) mpaka nje na jamii nzima inayo kuzunguka.
Kwa kuwa Suhala hili hutugusa kama sehemu ya maisha, Hivyo hii page ipo na inalenga lifestyle mbalimbali tunazozitumia katika kuendesha maisha ya kila siku, na hivyo tutapata mda wa kujifunza issue mbalimbali za kimaisha kama wanafamilia na watu ambao tunapenda kujifunza mambo mapya kila siku katika kuboresha maisha yetu.
Watu hupenda sana kuwa inspired katika maisha, hii pia ni changamoto, huwa napenda kutoa kile nilichonacho kama ushauri au mbinu flani ili kila moja wetu aweze kuchukua lake na limsaidie katika kujifunza, kurekebisha, kujenga na hata kuboresha pale anapoona pana umuhimu wa kufanya hivyo.
Kama Mwanamke kwenye page yetu ya My lifestyle nitajaribu kuzungumzia masuala mbalimbali katika mada zinazo husu maisha, kwa wote, kwa sababu inalenga familia kwa ujumla ambayo sehemu kila moja wetu hujengeka kimaisha.
Hivyo basi My LifeStyle imelenga kujadili masuala mbalimbali ya nayohusu Afya, Mapishi na Vyakula, Mahusiano, Jamiii, Uchumi, Elimu, Saikolojia na mengine mengi.
Pia My Lifestyle itatoa ushauri wa kimaisha katika majadiliano ya moja kwa moja kwenye page au private kwa mhusika,pia inalengo la kusaidiana na kukuza upeo wa kila mmoja kwa namna anavyo yastafisiri maisha na changamoto zake.

FASHION IN COLOR OF THE YEAR 2015, MARSALA PANTONE.
Red Carpet moments.



Lace details on this elegant Dress.

Make Up and other Accessories Idea.



JINSI YA KUTENGENEZA JUICE YA MBOGAMBOGA NA MATUNDA(VEGGIE JUICE).


Juice ni kinywaji ambacho hutengenezwa na matunda au mboga mboga halisi kabisa, watuwengi hupenda juice na ni nzuri kwa watoto pia kwani inafaida nyingi kiafya na pia husaidia kupunguza kasi ya kushambuliwa na magonjwa mbali mbali mwilini.

Veggie Fresh Juice nijuice inayotengenezwa na matunda na Mbogamboga isiyo wekewa aina yoyote ya kemikali, juice hii pia unaweza ukaitengeneza mwenyewe nyumbani kwa matumizi ya familia, haina gharama sana na pia ni rahisi kama utakuwa unatumia Brenda kwa ajili ya kusagia.


Leo tutaona jinsi ya kutengeneza Juice ya matunda na mbogamboga kama ifuatavyo.

Ingredients (Mahitaji)
  • 1 cucumber-Tango
  • 2 apples
  • 6-8 leaves kale -Majani ya Kabeji
  • 1/2 lemon-Limao
  • 1 tbsp ginger-Tangawizi
Directions (Jinsi ya Kuandaa)
  1. Wash all produce well- Osha Vizuri vifaa vyako na matunda na mboga mboga kwa maji safi yaliyo chemshwa.
  2. Peel the lemon, optional-Pili Menya Limao (sio lazima) na katakata vipande na vipande vya tangawizi.
  3. Juice-Changanya mchanganyiko wote kwenye brenda saga tayari kwa kuwa Juice.
  4. Pour over ice- Andaa vibande vya barafu tia kwenye Juice tayari kabisa kwa Kunywa.
  5. Enjoy!



NOTE:Zingatia kwamba unaweza kutengeneza Veggie Juice kwa matunda au mboga nyingine nyingi, mfano: Unaweza Tumia Spinach, Karoti, Nyanya, Green Apple, Lemon, Tango na Tangawizi.
Pili unaweza Tengeneza kwa kutumia Tango, Tikiti maji,Spinach na Nanasi Kidogo.

Faida za Veggie Fresh Juice.

Zipo faida nyingi sana za Veggie Fresh Juice katika mwili wa binadamu, hii ni pamoja na kukupa afya, kupunguza acid na kemiko chafu kwenye mwili, na Kukulinda na Magonjwa shambulizi ya mwili.




15th November,2014

SIMAMA NA TETEA HAKI YA MWANAMKE.


Leo nataka tuzungumzie ishu ya haki ya mwanamke na jinsi jamii yetu inalionaje hili suala na kwa namna au kiwango gani imeweza kusimama na haki za mwanamke, mwanamke ni nguzo katika familia hadi katika jamii na taifa kwa ujumla, ni mtu ambaye hujishughulisha na masuala mengi yakiwemo ya kifamilia na kijamii katika masuala ya kiuchumi na mengine mengi.

Majukumu yote haya mwanamke amekua pia mzazi na mlezi katika familia zetu, amekuwa mwenye kujishughulisha kila siku ili kuhakikisha analea familia katika hali nzuri nikimaanisha hasa watoto.

Hivyo basi kama binadamu mwanamke anastahili haki zote kisheria, na hili si jambo geni kwani hata Umoja wa mataifa umeweka kipengele hichi wazi kuwa mwanamke anahaki sawa na mwanaume, kakika masuala mbalimbali kama elimu,kazi,biashara,umiliki, na mengine mengi.



Wanawake wamekuwa wakikumbana na changamoto mbalimbali katika kuzifikia au kuzipata haki zao za msingi na hii inatokana na sababu nyingi ikiwemo kutotambua haki zao kutokana na elimu hii kutokuwepo nayo, napia inawezekana ni dhuluma ama uonevu unaofanywa na watu wengine kwa misingi ya dini ama siasa, au inaweza kuwa jamii tumejisahau kuwa ni wajibu kusimamia na kutetea haki zao.

Kuna matukio mengi  yameripotiwa au tunayaona wenyewe kwa macho katika maeneo tunayoishi unyaswaji wa wanawake au uvunjifu mzima wa haki za wanawake ukifanywa na watu au mtu na kunyamaza kimya, wengi tumekuwa tukiogopa, ila hii haitosaidia kwani mwisho wasiku tunaona wanawake wakitekea kwa kufanywa vilema au kufa kwa sababu hizo.

Kila mtu anajukumu la kubadilika na kusimamia haki za wanawake zifuatwe ili kupunguza uonevu,unyanyasaji na udhalishwaji kwa wanawake.


29th October,2014

                                                  

10 Best Natural ways to glow your skin/ Njia 10 Asilia za kusaidia Ngozi yenye Afya.

Katika maisha yangu, nina hisi na wengine pia, huwa tunapenda ngozi yenye Afya, nikimaanisha Ngozi isioweza kushambuliwa na Bacteria mbalimbali ama magonjwa ya ngozi kiurahisi..leo kidogo nimejikita hasa kwenye Ngozi ya Uso, yaani Usoni, ambapo huwa tuna shambuliwa na chunusi za mara kwamba, mba na ukavu wa ngozi.

Nimeelewa umuhimu wakuwa na ngozi ya uso yenye afya kwa njia salama zisizo na madhara ya njia asilia zaidi, hii nikusaidia kutopoteza muda na madawa au cream zilizo na gharama, kwenye vipodozi ambavyo vina kemikali.

Hizi hapa ni njia salama na rahisi kuzifanya ukiwa nyumbani kwako kutengeneza kipodozi chenye kutia afya ngozi yako ya usoni.

1) Tomatoes for good skin/Matumizi ya Nyanya.

tomatoesDid you know that tomatoes can give you fresh and healthy skin? Not just that, tomatoes can also be effective when it comes to curing pigmentation and removing stubborn acne marks.
Rubbing raw tomatoes on your face not only helps reduce sun tan and damage but it also helps you get back your lost glow.
Here is how you can make a quick face pack using tomatoes. All you need is tomato and a lemon. Squeeze the juice from the tomato and lemon into a bowl.  Mix them together really well with a spoon. Apply this mixture carefully under your eyes before you wash your face.

2) Cucumber and limejuice for healthy skin/ Tango

cucumber-and-lime-juice

Take 2tsp cucumber juice, 2tsp limejuice and 2tsp rose water. Mix it well and apply this mixture after washing your face. Keep it overnight and wash it in the morning. It clears the complexion of the skin and helps to keep the skin healthy.

3) Milk, salt and limejuice/ Juisi ya Limao

milk-lemon

Take 50 ml. of raw milk, a pinch of salt and 2tsp of limejuice and mix them well together. Use it as a cleansing lotion. It cleans the deep pores of the skin. We can apply this mixture not only to your face but also for your other parts of body like arms, legs etc. After a few weeks of doing this your skin will be silky smooth and glowing.

4) Turmeric powder, Wheat flour and Sesame oil

Turmeric-wheat-flour-seasme-oil
Make paste from equal quantities of turmeric powder and wheat flour with sesame oil. Apply this paste to the face. Keep it till paste dries and then wash the face gently. This process helps to remove the unwanted hair of the face. It is a very traditional paste used in ancient times, This paste should apply daily for better skin. Specially in winter season,  to avoid dryness of skin.

5) Orange juice/ Chungwa

orange-juice
Take 2-3tsp of orange juice and apply it to the face by using cotton piece. It helps to make the skin soft and smooth. Orange juice is very healthy for inner body as well as for outer body. We can make another face mask by adding 1tsp of baking soda in 1tsp of orange juice, use brush to apply all over face and leave on for 15 minutes. Using circular motions, gently scrub in to skin then rinse off and pat dry with a towel. This helps get rid of your blackheads and leaves your skin smooth and soft.

6) Cabbage juice and honey/ Asali na Kabeji

cabbage-juice-honey

Take 1tsp of honey and mix it with 30ml of cabbage juice. Apply this mixture regularly and consistently to keep the wrinkles away and keeps the skin healthy.

7) Raw Carrots

raw-carrots
Make a fine paste of raw carrots and apply it to the face. Keep it for one hour and wash the face. See the magic and you will get a wonderful glowing skin. carrots are good for acne. We can make another face pack by using 2tsp of blended carrots and 1tsp of honey and mix it well then apply this mask on the face. Rinse it off after 10 minutes. This mask lightens the dark skin and helps to treat the dry skin

8) Limejuice, glycerin and rose water/ Waji ya ua waridi.

lime-juice-rose-water-glycerinr
Take equal quantities of limejuice, glycerin and rose water. Mix it well and apply this lotion to the face regularly at bedtime which is very useful and helps to get rid of the pimples, blackheads and other blemishes. It also helps to make your skin soft. This lotion can also be applied to other parts of the body like hands, feet etc.

9) Tomato, Lemon juice and Whipping cream or natural yogurt

tomato-yogurt-lemon-juice

Take half of a tomato and squeeze the juice out, add ½ tsp lemon juice, 1tsp of whipping cream or yogurt and mix it well. Then apply this mixture to the face. After 15 minutes, rinse off the mask with water. Don’t waste the tomato pulp, mash it up and use it as a cleanser. It makes an excellent skin cleanser. It reduces the blemishes, softens wrinkles and fine lines, improving skin’s overall texture.

10) Lemon juice and honey

lemon-juice-honey

Squeeze half a lemon in to a bowl, mix with 2tsp of honey and stir until it turns out to a golden liquid. Now apply this mixture on the face and relax for 10-15mins. Do not talk or move your face during this time. Relax as the skin hardens, then wash the face with cold water and gently scrub with the hands. Gently dry the face and feel the glowing softness of the skin.

Unaweza soma zaidi, inapatikana--  http://xbestthings.com/10-best-natural-ways-glow-skin/




21st October, 2014

PANUA MAARIFA ONGEZA UJUZI KATIKA MAISHA KWA KUWA NA TABIA YA KUJISOMEA VITABU.

Watu wengi tumekuwa hatuna mazoea na taratibu za kujisome vutabu, majarida na magazeti, hii nikutokana na mpangilio usio mzuri wa kimaisha nakuona kufanya hivyo nisehemu ya kujipotezea muda.
Kama binadamu ni vyema kuwa na mazoea ya kujisome chochote na hata ikiwa ni BIBLIA au Kitabu chochote kile cha dini yako, hii husaidia mambo mengi katika maisha, ukiweka kando umri wako.



Panga na jitambue unapenda aina gani ya vitabu vya kusoma, na pili kuwa na maono ya kujifunza na kukuza upeo wako kupitia vitabu hivyo, Mfano mzuri ni mimi mwenyewe huwa napenda vitabu vinavyonijenga kimaisha hasa jinsi ya kukabidhiana na changamoto mbalimbali za maisha na vile ambavyo huzungumzia makuzi mzuri ya mtoto.
Hivyo basi ni vyema kuwa na utaratibu wa kununua vitabu na jiwekee kabisa budget hii iwe mazoea ili usiweze kukosa kile unachokipenda kutoka kwenye vitabu.



Kuna aina nyingi ya vitabu mfano vinavyohusu maisha na changamoto zake, mahusiano, mapichi na vyakula, afya na n.k.
ambapo ukiwa nimtu wa kusoma utajikuta unainuka na kuongeza maarifa flani ambayo yatakusaidia kwa namna moja au nyingine katika maisha.

Kwanini basi tunashauriwa kusoma vitabu.

Kwanza husaidia kujifunza vitu vipya vya kimaisha kwa ujumla, pili Hujenga CONFIDENCE/KUJIAMINI kwa mtu, hutuimarisha kiakili zaidi, husaidia kukuza uwezo wa kutoa MAAMUZI.



Pia husaidia kupunguza stress za maisha na kiakili kwa sababu kunaina ya vitabu tutoa relief kwa comedy ambazo huwemo kwenye vitabu hivyo, vile vile hukuza uwezo wa KUMBUKUMBU, na kuimarisha LUGHA kwa kupitia misamiati mipya unayo kutana nayo kila mara unaposoma vitabu.


MAZOEZI MEPESI YA VIUNGO KWA KILA SIKU ASUBUHI.

Kuna mazoezi mengi mepesi kwa mtu ambaye ndio mara ya kwanza katika mazoezi, hii ni pamoja na kujaribu kufanya mazoezi ya viungo angalau mara moja kwa siku yaani Asubuhi.


Mazoezi ya haya huweka viungo kuwa karika hali ya uchangamfu, unaweza kutembea, kukimbia taratibu, kucheza mziki kwa hatua, au kufanya YOGA.

Mazoezi ya kutembea na kukimbia taratibu yanaweza fwanya barabarani au gym inategemea unapendea wapi. ila ni vyema ufanye barabarani ili uweze kupata refleshment ya fresh air na kushangaa kidogo kitendo kitacho kupa nguvu pale unapo hisi umechoka.



Kucheza mziki hasa mziki wa RUMBA, ni sehemu nzuri ya kwa wanaoanza mazoezi, kusaidia kufanya viungo kuwa active kwa mazoezi zaidi, ufanya mwili kuwa pia mwepesi, hii huweza fanya nyumbani au gym.



Yoga pia nimazoezi zoefu kwa kila mtu hasa mwepesi, hunyoosha misuli ya mwili na tutoa relief /stress za za misuli ya mwili na akili pia.



9th october,2014

JINSI YA KUTUNZA NA KUTHAMINI MUDA.

Katika Maisha watu wamekuwa wakilalamika kuwa sina mda sina mda, hata katika mambo muhimu sana wamekuwa wakijikuta wanashindwa kuyatekeleza kutokana na mpangilio mbovu wa ratiba na mda walionao.
Mda ni kitu mhimu sana katika maisha haya ya sasa, kila kitu huenda na muda hata kama wewe unaona si chamuhimu ila kwa mwenzako ni chathamani sana, hivyo basi nivyema kujali mda na kuuthamini.
Hizi hapa kuna baadhi ya mbinu na hatua za kuzifuata zinazoweza kukusaidia kutunza muda wako na kufanya vitu vyote unavyovipanga ndani ya mda.
 
1. Kwanza kabisa Jifunze kuandaa na ratiba ya siku nzima kila siku iwe ni mfanyakazi, au mwanamke unayeshinda nyumbani, jitahidi kuandaa ratiba ya nyumbani kwako kipi kifanyike na kwa mda upi.

2. Pili Jaribu kuwahi kuamka mapema kama unakuwa ni mtu mwenye shughuli nyingi, wengi tumekuwa wavivu wa kuwahi kuamka na kujikuta tunakuwa nyuma ya muda sana.

3. Jitahidi kuwa mkweli na mda na unachokifanya, usifanye kitu pasipo kuwepo kwenye ratiba, kama hakina umuhimu kwa wakati huo.


4.Na mwisho Pata muda wa kutosha kupumzika vizuri kusaidia kufanya kazi vizuri, hii ni sehemu muhimu kwa sababu watu wengi wamekuwa wakifanya vibaya katoka shughuli zao kwasababu ya kufanya kazi nyingi bila mpangilio na wakati huo wakiwa wamechoka.


Hope tumejifunza kitu hapa, kuhusu jinsi ya kutunza muda na kufanya shughuli zote ndani ya muda.

WOMEN'S HEALTH

Hii ni sehemu wanawake wengi hupenda kuizungumzia sana siku hizi, Afya ya mwanamke ni sehemu yenye mada nyingi ndogo ndogo ndani yake ila hapa nataka kuona afya ya mwanamke kwenye chakula anachokula na matokeo yake, na jinsi ya kutengeneza mwili ulio-fit wakati wote.



Wengi wanawake tumekuwa tunalalamika mara kwa mara kuhusiana na maumbo yetu na afya kwa ujumla kutokana na vyakula kunavyokula, tumekuwa tunajionea matokeo yasio ridhisha ya vyakula bila kujua ya kuwa ni vyema kuwa na mpangilio wa kipi cha kula kama mwanamke na katika kipindi kipi.



Mfano, kuna wakina mama wajawazito hawa huwa wanahitajika kula vyakula vyenye virutubisho kwa wingi, na mara nyingi huwa wanahisi njaa na hivyo kuwalazimu kula mara kwa mara, then kuna wakati umesha jifungua na unanyonyesha hapa pia wakinamama huwa wanakula kwa wingi kutokana na unyonyeshaji, hii ni kwasababu huitajika kutengeneza maziwa mengi na yenye virutubisho kwa mtoto.


na ,mwisho ni kipindi cha kumwachisha mtoto kunyonya je kama mama unapangaje ratiba ya kula sasa? hapo ndipo tunapokose na kujikuta tunajiachia nakujisahau, kwanza kabla ya ujauzito nivyema kujua afya yako kama mwanamke ya kwamba ipo kipindi utabeba mimba na utajitunza vipi, na baada ya hapo utachukua jitihada zipi kujiweka katika afya na mwili ulio-fit.

NOTE: Usipende sana kuzungumzia suala la kukonda au kupungua, wewe angalia suala la kuwa na afya nzuri na kuwa fit kimwili (fit-body).

Zingatia Utaratibu wako wakuwa na ratiba ya mazoezi mbalimbali na Kujitahidi kula vyakula vyenye afya ambavyo havita ongeza uzito mkubwa kwenye mwili, havita ongeza mafuta sana kwenye ngozi na kuharibu mwonekano mzima wa afya yako.

Kuna vyakula vingi vyenye kumletema mwanamke umbo zuri lenye kumwezesha awe free akiwa popote na vazi lolote. Wanawake tunapenda kuvaa na tuvae nguo zitupendeze au kutupa mwonekano mzuri, basi ni vyema kujitahidi kujua ni nini unatakiwa kufanya ikiwa nikuweka ratiba nzuri ya vyakula na mazoezi ya mara kwa mara ya viungo. Katika mada zijazo tutangalia ni jinsi gani tunaweza ona aina hizo za vyakula na tips mbalimbali za fitness kwa afya ya mwanamke.

No comments:

Post a Comment

Blog Comments

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...