Wednesday, 18 September 2013

Tips on how to Design, Organize and Decorate your Dressing Room!

Hello wapendwa na wadau wa Blog yetu ya Whitewings Home Decor, leo ningependa tuzungumzie jinsi ya kuweka dressing room katika hali nzuri hii nipamoja na kupanga kabati lako la nguo na kuhifadhi vipodozi vyako katika hali ya usafi hasa kwa wale wenye dressing table..ni vyema kujua nikiasi gani cha nguo na aina gani ya  nguo ulizonao ili kujua nijinsi gani utachagua kabati la nguo kwani kuna aina nyingi ya makabati..mfano kwa wanawake wengi huwa wananguo na viatuvingi sana hivyo ni vyema kutengeneza kabati kubwa na hata kama ni dogo ni vizuri kuzingatia upangaji mzuri wanguo zako kulingana na aina ya nguo, viatu, mapochi, mikanda ya nguo na vingine vingi!







Pia kwenye Dressing Table ni vyema kudesign kulingana na matumizi yako..weka kioo kikubwa chakutosha kujitazama na pia dressing table yako iwe na drawer za kutosha uhifadhi vipodozi  kuzingatia pia aina ya vipodozi/ cosmetics unazotumia hii ni kutokana huwezi kuweka kila kitu juu ya dressing table yako..weka pia accessories zako mfano..pete, ear-rings au bangili zako kwenye pochi maalumu kisha hifadhi kwenye droo! hii husaidia zisiharibike kwa urahisi au kuibiwa kama itatokea, pia hifadhi vifaa vya kutengeneza nywele kwenye drawers mfano machanuo na vibanio!
 












Kila mwanamke hupenda nyumba ipendeze basi zingatia pia ku-decorate Dressing Table yako kwa kuweka hata chupa ya ua zuri juu yake..frame ya picha au other accessories..!
 


No comments:

Post a Comment

Blog Comments

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...